Urusi na Ukraine: Baadhi ya raia wa Afrika Mashariki walioko Ukraine na wazazi waelezea hisia zao
Milipuko mikubwa na mashambulizi ya anga imeshuhudiwa kote mjini Kyiv wakati vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vikiingia siku yake ya pili.
Maafisa wa Ukraine wamesema Urusi imefanya mashambulizi zaidi ya makombora kuzunguka mji mkuu.
Picha za video zimeonyesha kitu kikubwa -- ama ndege au kombora -- kikianguka kutoka angani baada ya kupigwa risasi.
Maelfu ya watu mjini Kyiv wamekaa usiku kucha katika kituo cha gari moshi ili kujikinga na tishio la mashambulizi ya anga.
Baadhi ya raia wa kutoka Afrika mashariki wanaelezea hisia zao kufuatia vita vya Urusi dhidi ya Ukraine kuingia siku yake ya pili. Mwandishi wa BBC Martha Saranga amezungumza na wanafunzi Watanzania ambao wapo masomoni nchini Ukraine na pamoja na wazazi wa baadhi ya wanafunzi ambao ni raia wa Kenya.