Moise Kabagambe :Kwa nini mauaji ya mhamiaji huyu kutoka DRC yamezua hamaki Brazil?

Maelezo ya video, Moise Kabagambe :Kwa nini mauaji ya mhamiaji huyu kutoka DRC yamezua hamaki Brazil?

Mamia ya wananchi nchini Brazil walijitokeza kuandamana kushinikiza haki kutendeka dhidi ya mauaji ya kijana Moise Kabagambe mwenye asili ya Kiafrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)

Moise aliuawa nje ya kibanda alichokuwa akifanyia kazi ambapo jamaa wanasema sababu iliyopelekea mauaji yake ni alipokwenda kudai fedha kwa mwajiri wake .

Mapema mwezi huu Watu 3 walikamatwa nchini Brazil kwa mauaji ya Moise,baada ya mauaji yake kunaswa kwenye video, na kusababisha hasira ya umma.

Mwandishi wa BBC Roncliffe Odit anasimulia mkasa mzima wa kilio cha kijana huyo