Kiongozi wa upinzani wa Tanzania Tundu Lissu amemwambia Rais 'ninataka kurudi nyumbani'
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na kiongozi wa chama cha upinzania na makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu anayeishi uhamishoni mjini Brusssels, Ubelgiji kwa sasa. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilisema kwa kifupi kuwa wawili hao walizungumza juu ya masuala mbalimbali yenye maslahi na ustawi wa Tanzania.
Mwandishi wa BBC Scolar Kisanga amefanya mahojiano na Tundu Lissu na kwanza amemuuliza kwamba ni nini hasa walichokizungumza?