Mjane wa Maalim Seif: Mama Aweina aeleza jinsi wanavyomkumbuka mwaka mmoja baada ya kifo
Wiki hii, Tanzania bara na visiwani Zanzibar itaadhimisha mwaka mmoja tangu kufariki kwa kiongozi na mwanasiasa mashuhuri katika siasa za Tanzania Maalim Seif Sharif Hamad.
Huku kukiwa na maandalizi ya siku yake ya kufariki ambae ni tarehe 17 mwezi, Mwandishi Wetu Aboubakar Famau amemtembelea mke wake maarufu kama mama Aweina na kufanya nae mahojiano nyumbani kwake Unguja na kwanza alimuuliza ni kitu gani hasa ambacho wanamkumbuka nacho Maalim licha ya kwamba hamko nao?