Hatua ya kufunguliwa magazeti manne Tanzania yasifiwa na wadau nchini humo
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania Nape Nnauye ametoa leseni kwa magazeti manne ambayo yalikuwa yamefungiwa kwa mjibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.
Waziri wa habari nchini Tanzania, ametoa leseni ya vyombo kuanza kufanya kazi, wakati alipozungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali ya habari nchini humo .
Katika hatua nyingine Waziri Nape ameitaka Idara ya Habari Maelezo kushirikiana na wahariri na taasisi nyingine za habari kuandaa kikao cha kujadili marekebisho kuhusu sheria ya habari.
Simon Mkina,ni mmiliki wa gazeti la MAWIO miongoni mwa magazeti yaliyofunguliwa na hapa anaelezea namna alivyopokea tangazo hilo
Nalo baraza la habari Tanzania MCT,na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA TAN wametoa nyaraka zao za kupongeza hatua hiyo ya serikali kuvifungulia vyombo hivyo vya habari na kuelezea matumaini kwa hatua kufanyiwa marekebisho kwa sheria kandamizi katika uhuru wa habari.