Rais Samia aagiza maafisa wa serikali kukutana na viongozi na wakaazi wa Ngorongoro

Maelezo ya video, Rais Samia aagiza maafisa wa serikali kukutana na viongozi na wakaazi wa Ngorongoro

Serikali ya Tanzania imeeleza kuwa itakutana na wananchi wanaoishi katika Hifadhi ya Ngorongoro na Loliondo kwa lengo la kuwasikiliza na kuwaelimisha ili kumaliza migongano iliyopo kwenye hifadhi hizo.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameagiza viongozi wa serikali yake kukutana na viongozi mbalimbali wa maeneo ya Ngorongoro na wananchi wa eneo hilo ili kumaliza sakata hilo.

Mjadala mkali uliibuka katika bunge la Tanzania baina ya wabunge wakati wa kuchangia taarifa ya utekelezaji wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.