Mchekeshaji Eric Omondi wa Kenya atetea mbinu zake za ‘kuwatetea’ wasanii nchini humo

Maelezo ya sauti, Mchekeshaji Eric Omondi wa Kenya atetea mbinu zake za ‘kuwatetea’ wasanii nchini humo

Mchekeshaji wa Kenya Eric jana alizua sintofahamu nje ya majengo ya bunge nchini Kenya baada ya kujifungia katika kisanduku akilenga kuwashinikiza wabunge kupitisha mswada wa kuhakikisha asilimia 75 ya nyimbo na kazi za wasanii wa Kenya zinapeperushwa na vituo vya habari nchini humo .

Omondi ambaye amekuwa akiendeleza harakati zake kupitia visa kama hivyo amesema ataendelea kupigania haki za wasanii wa Kenya licha ya kushtumiwa na baadhi ya wakosiaji wake kwamba hatua zake hizo ni sarakasi za kujipatia umaarufu na sifa .

Akiongea na BBC Swahili Omondi amesema hataovunjwa moyo na ukosiaji huo kwani anachopigania kitawafaidi wasanii wanaochipuka

Miezi miwili iliopita mcheshi huyo alikamatwa alipokuwa akijaribu kuvamia bunge kwa suala hilo hilo.

‘’Nilipokuwa hapa siku za nyuma , nilisalia peke yangu , hakuna msanii hata mmoja wa muziki alinisaidia kupigania maslahi yao’’, Omondi alilalama.