Wavulana wa Nigeria: Kuanzia kuchukua filamu kwenye simu hadi kuwa maarufu Netflix

Maelezo ya video, Wavulana wa Nigeria waliovuma Netflix kwa kutengeneza filamu za kisasa

Wavulana tisa katika mji wa Nigeria wa Kaduna walianza kufanya jaribio la kutengeneza filamu za kufikirika mwaka 2016.

Waliazima simu za smartphones kwa watu wa familia zao, na kutengeneza kifaa cha kushikia simu cha mbao wakati wanapiga picha za video.

Miaka mitatu baadaye, walipiga picha za filamu fupi iliyopendwa, na kuwafanya mamilioni ya watu, waiwemo nyota wa Hollywood. Mwandishi wa BBC Damilola Oduolowu alikutana na watengenezaji hawa wadogo wa filamu nchini Nigeria na hii ni simulizi yao.