Kemikali za sumu zinavyoathiri wachimba madini Tanzania

Maelezo ya video, Kemikali za sumu zinavyoathiri wachimba madini Tanzania

Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), wakati uchimbaji madini unaajiri karibu 1% ya nguvu kazi duniani, sekta hiyo inasababisha 8% ya ajali zinazoleta vifo.

Hata hivyo watu wengi wanapata madhara ya kiafya ya muda mrefu kutokana na kazi yao ya uchimbaji madini katika maisha yao ya baadaye wakati mwingine hurithisha hadi kwa vizazi vijavyo.

Dayo Yusuf alitembelea mgodi wa dhahabu Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo wachimbaji wadogo hukimbilia dhahabu licha ya hatari kwa afya zao.