Atupele Sanga: 'Nililia sana nilipoambiwa siwezi kupata kazi kisa sijasoma'

Maelezo ya video, Atupele Sanga: 'Nililia sana nilipoambiwa siwezi kupata kazi kisa sijasoma'

Katika mfululizo wa makala kuhusu vijana walio chini ya umri wa miaka 30 ambapo huangazia vijana waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika teknolojia, siasa na kijamii kwa nchi za Afrika Mashariki.

Leo tunae Atupele Sanga maarufu kama @recho_interiorsdesgn ambaye ni binti mwenye umri wa maka 23 aliyejidhatiti katika ufanyaji kazi bila kujali fikra potofu juu ya kazi ya mwanaume na kazi ya mwanamke kwa kufanya kazi ya uwekaji mapambo katika nyumba.

Amepitia mengi kama mwanamke hasa ukizingatia ni ulimwengu wa kazi za kiume ambapo ni nadra sana kuona mwanamke akijishughulisha nazo.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amemtembelea @rechodecoration katika eneo lake la kazi ambapo akapata wasaha wa kufahamu mengi yanayomsibu shujaa huyu mpambanaji.