Goodluck Salema: ‘Natamani nimvalishe msanii Diamond Platnumz'
Katika mfululizo wa makala kuhusu vijana walio chini ya umri wa miaka 30 ambapo huangazia vijana waliofanya vizuri na wanaoendelea kufanya vizuri katika teknolojia, siasa na kijamii kwa nchi za Afrika Mashariki.
Leo tunae kijana @_luckie Mwanafunzi na mbunifu kutoka Tanzania mwenye umri wa miaka 21 anayejishughulisha na ujasiriamali akijikita katika ubunifu wa mavazi ya kimuundo ambapo huunda upya Jeans kwa kuongeza nakshi na kuzifanya zivutie zaidi.
Akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu akisomea ‘Business Administration’ amekuwa akiwafundisha vijana wenzie kazi hii, sasa ana vijana wawili anaoshirikiana nao kikazi, akiwa na ndoto za kufungua kiwanda kwaajili ya kutengeneza nguo za kimuundo kitakachowawezesha vijana wengi zaidi kujiajiri na kukuza vipaji vyao.
Anasema kuna nguo huzivaa chuoni na wengi humcheka na kumshangaa kutokana na mitindo yake kuwa ni ya kipekee sana.
Mwandishi wa BBC @frankmavura amemtembelea kijana huyu ambaye anasema uhaba wa wateja na watu kutomuelewa katika kazi zake hakujamkatisha tamaa kwani anaendelea kupambana mpaka afikie malengo aliyojiwekea.
#bbcswahili #30under30 #vijana #ajira #tanzania #biashara #wabunifu #ubunifu