Kukulia gerezani: Watoto wanaamini gereza ni nyumbani
Nchi nyingi kote duniani huwaruhusu watoto kuishi na mama zao waliofungwa gerezani.
Hatahivyo, suala hilo ni tata, huku baadhi ya watu wakidai kuwa gereza sio mazingira mazuri ya malezi kwa mtoto.
Nchini Kenya watoto wapatao 200 kwa sasa wanaishi magereza ambako mama zao wanatumikia kifungo na suala hili limeibua mjadala nchini humo juu ya ni hatua gani zinazofaa kuchukuliwa kuwasaidia watoto hao. Mwandishi wa BBC Agnes Penda ana taarifa zaidi.