Kutana na babu wa miaka 84 anayewashangaza wengi kwa kunyanyua uzani
Brian Winslow mwenye umri wa miaka 84-ni mnyanyuaji uzani kutoka Derbyshire, Uingereza.
Bw. Winslow, ambaye huenda kwenye mazoezi mara sita kwa wiki, anasema alivutiwa na unyanyuaji uzani alipokuwa akifanya kazi zama za ujana wake.
Kulingana na yeye, umri si hoja mtu anapofuatilia anachopenda
Amefuzu katika mashindano ya Chama cha wanyanyuaji uzani wa Ungereza wasiotumia dawa nza kuongeza nguvu dhidi ya wanyanyuaji wenginne wa uzani kutoka maeneo tofauti nchini Uingereza.