Eliud Kipchoge: Mwanariadha wa mbio za Marathon

Maelezo ya video, Eliud Kipchoge: Mwanariadha wa mbio za Marathon

Mwanariadha wa mbio za Marathon

Anadaiwa kuwa mwanariadha bora zaidi wa mbio za marathon mwaka huu, Eliud Kipchoge aliimarisha hadhi yake zaidi katika maili 26.2 baada ya kushinda dhahabu yake ya pili ya Olimpiki katika mashindano hayo.

Akiwa mtu wa tatu kufanikiwa kutetea taji la Olimpiki , raia huyo wa Kenya baadaye alichaguliwa kuwa mwanariadha bora wa kiume na kamati ya kimataifa ya michezo ya Olimpiki.

Ushindi wake mjini Tokyo una maana kwamba ameshinda mara 13 kati ya mbio 15 za Marathon alizokimbia tangu alipoanza kukimbia mbio hizo 2013 , huku akijiongezea sifa za kuvunja rekodi ya dunia ya 2:01:39 aliyoweka mjini Berlin 2018.

Akiwa na umri wa miaka 36, alikuwa mwanariadha mwenye umri mkubwa zaidi kushinda taji la Olimpiki tangu mwanariadha wa Ureno Carlos Lopes wakati huo akiwa na umri wa miaka 37 mwaka 1984 na kupata uhsindi mkubwa zaidi tanagu 1972.