Hatari ya mafundisho potofu kuhusu mahusino ya ngono mitandaoni
Mafundisho kuhusu mahusiano na ngono shuleni huibua mjadala ,lakini daktari mmoja huko Wales Uingereza anasema Watoto kuanzia umri wa miaka kumi na moja wanajifunza kupitia mitandao na video za ponografia na kuptoshwa kuhusu ngono.
Dk Kate Howells ana wasiwasi kwamba ukosefu wa maelezo katika mipango ya mtaala mpya wa elimu ya ngono na uhusiano unasababisha hatari kwa kizazi kichanga.
Hivi unadhani mafundisho ya mahusiano na maswala yanayoandamana na ngono yatapunguza hatari ya Watoto kupotoshwa na ponografia mitandaoni? Sema nasi kwenye facebook BBC Swahili