Kuwasaka 'wadukuzi mamilionea' wa Urusi
Baada ya mwaka usio na kifani wa mashambulizi mabaya ya kimtandao, shinikizo za kimataifa zinaendelea dhidi ya wadukuzi.
Magenge ya wadukuzi yanakamatwa katika nchi nyingi, lakini sehemu moja ambapo watu hawashiki ni Urusi - ambayo kihistoria imepuuza shutuma za kuwahifadhi baadhi ya wahalifu wabaya zaidi wa kimtandao.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya mtandao Joe Tidy alisafiri hadi Urusi ambapo baadhi ya washukiwa wanafurahia utajiri wao bila juwa na hofu ya kukamatwa.

