Mabadiliko ya tabia nchi: Mbolea zilivyosababisha moto kuwaka chini ya ardhi
Wakati dunia ikipambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, Joto lililozidi kwenye Mboji (Takatakata za mimea na wanyama zilizooza chini ya ardhi (Organic Material) ndio chanzo kilichosababisha moto kuwaka ardhini katika eneo dogo la kijiji cha Mrao Wilayani Rombo Kilimanjaro na kuzua taharuki kubwa, miezi michache iliyopita.
Tayari wataalamu wa Jiolojia wanasema eneo hilo ni salama sasa kutokana na joto hilo kuwa si la volcano.
Mwandishi wa BBC Frank Mavura alitembelea eneo hilo kujionea hali ilivyo kwa sasa na hofu iliyowakumba wanakijiji wakati wa tukio