Gambia ina jua la kutegemewa, lakini ni kwanini hailitumii kuzalisha nishati?

Maelezo ya video, Ni kwanini Gambia haiwezi kunufaika na nishati ya jua?

Wagambia huzalisha nishati mbadala kibinafsi kwasababu hawawezi kutoshelezwa na nishati ya mifumo ya umeme ya taifa.

Serikali inasema hakuna sera iliyopo ya kudhibiti bei na kuifanya iendelee kuwa ya chini. Lakini inahangaika kujaribu kuondokana na mafuta machafu.

Serikali imejiwekea lengo la kufikia kiwango cha sifuri cha utoaji wa hewa chafu ifikapo mwaka 2050. Na wakati ikitengeneza mabwawa mapya ya nishati ya maji, pia inataka kuchimba mafuta.