Muigizaji wa vichekesho Tanzania ajivunia uhusika wake wa kike
'Napenda kuigiza uhusika wa kike ingali mimi ni wa kiume' anasema Abdallah Sultan maarufu kama Dullvani ambaye ni muigizaji wa vichekesho vya runinga nchini Tanzania.
Dullvani anatumia mtindo wa kuigiza akiwa na mavazi ya kike, jambo ambalo wengi wamekuwa wakiliona kama si kitu kizuri japo yeye mwenyewe anasema anapenda nakitu kinachomuingizia kipato hivyo hana budi kukifanya kwa juhudi na nguvu zake zote.
Mfahamu msanii huyu kupitia video hii iliyoandaliwa na mwandishi wa BBC ,Frank Mavura