Jinsi mwani wa baharini unavyosaidia wazazi kupeleka watoto shule
Pwani ya Kenya ina sifa za mchanga wake mweupe na fukwe za kuvutia watalii na walioko katika likizo.
Lakini chini ya mchanga huo kuna mwani wa baharini.
Mwani huo ni miongoni mwa vitu vinavyowapatia pato kubwa wakazi wa Shimoni , ambao huyatumia kutengeneza sabuni na Mafuta huku faida zake pia zikisadia kulipa karo shuleni.