Je dhana potofu kwamba chanjo ya corona ina sumaku ilitoka wapi?
Kanda za video za watu wakiweka sumaku katika maeneo waliodungwa chanjo za corona zimesambaa katika mitandao ya kijamii kama vile Tiktok na Instagram. Baadhi ya watu wanasema kwamba kuna kitu kama sumaku huku wengine wakiendelea na kusema kwamba kuna kibamba kidogo – dhana ambayo sio ya kweli..