Robert Dickson: Je muuza kahawa huyu kutoka Tanzania ndiye nadhifu zaidi barani Afrika?‘
Pengine umezoea kuona suti ikivaliwa na wafanyakazi wa ofisini ama maafisa wa serikali,la hasha mambo ni tofuati kwa Robert Dickson ambaye ni muuza kahawa.
Dickson anauza kahawa akiwa amevalia suti wakati wote wa kazi yake, jambo ambalo anasema baadhi ya watu hudhani yeye ni afisa wa serikali na si muuza kahawa.
Lakini ilikuaje akaanza kuvaa suti katika biashara yake hii?
Mwandishi wa BBC Frank Mavura alikutana na Dickson jijini Dar es salaam na kuandaa taarifa ifuatayo.