Shambulio la 9/11: Dakika 102 zilizobadilisha Marekani na ulimwengu

Maelezo ya video, Shambulio la 9/11: Dakika 102 zilizobadilisha Marekani na ulimwengu

Mnamo Septemba 11 mwaka 2001 Marekani ilishambuliwa.

Mtandao wenye msimamo mkali wa Kiislamu, al-Qaeda, uliteka nyara ndege nne na kuzitumia kama makombora dhidi ya maeneo maalumu ya Marekani.

Karibu watu 3,000 waliuawa. Marekani ilijibu janga hilo kupitia oparesheni iliyoitwa ‘vita dhidi ya ugaidi’ – iliyojumuisha uvamizi wa nchi mbili na kusabisha vifo zaidi.

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa asubuhi hiyo iliyobadilisha Marekani na ulimwengu.