Mzozo wa Afghanistan: Wakalimani wa NATO wahofia maisha yao baada ya Taliban kudhibiti Afghanistan
Wanamgambo wa Taliban wamechukua udhibiti wa maeneo yote ya Afghanistan na sasa wako mji mkuu wa Kabul. Maelfu ya watu wamekimbia makwao katika wiki chache zilizopita.
Wakalimani waliyokuwa wakifanya kazi na vikosi vya Uingereza na NATO kwa miaka 20 iliyopita, wana wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wao. Wanamgambo wa Taliban wanawaona kama wasaliti na wamekuwa wakitaka ufafanuzi kutoka kwa Uingereza kuhusu hatma yao.
Karibu wakalimani 1800 wa Afghanistan na familia zao ambao wamekuwa wakisaidiwa na Uingereza wamehamishwa katika wiki chache zilizopita na wengine wengi wanatarajiwa kuwasili nchini humo