Lifahamu kabila la Tanzania linalothamini senene kuliko nyama

Maelezo ya video, Je senene ni watamu kuliko Nyama?

Senene ni wadudu jamii ya panzi na wanapewa heshima kubwa katika jamii ya wahaya waliopo, Kagera magharibi mwa Tanzania.

Kwa Mila na desturi za jamii hiyo Senene hutumika kama zawadi muhimu wakati wa taratibu za Ndoa.

Wadudu hawa wanapatikana pia katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki kama Uganda na Rwanda.

Mwandishi wa BBC Munira Hussein alitembelea mkoani Kagera na kuandaa taarifa ifiatayo.