Nilimkatisha mwanangu kunyonya ili nimnyonyeshe mtoto wa dadangu aliyefariki dunia
Asha Aboubakar mkazi wa Ngusero jiji Arusha alilazimika kumkatisha kunyonya mwanae mwenye mwaka mmoja na nusu ili amnyonyeshe mtoto mchanga wa mdogo wake aliyefariki muda mfupi baada ya kujifungua
Akijua fika na baada pia ya kushauriwa na wataalamu faida ya maziwa ya mama amelibeba jukumu hilo kwa uaminifu licha ya changamoto kadhaa
Eagan Salla alimemtembelea mkoani Arusha wakati dunia ilipokuwa ikiadhimisha juma la unyonyeshaji na hii hapa taarifa yake