Mtanzania atengeneza jiko la umeme linalotumia mawe

Maelezo ya video, Mtanzania atengeneza jiko la umeme linalotumia mawe

Tegemeo Dickson Nzigo ni kijana wa Kitanzania kutoka mkoa wa Kigoma. Ametumia ubunifu wake kuunda aina ya jiko ambalo linatumia vipande vidogodogo vya mawe badala ya kutumia mkaa. Jiko hilo pia lina feni ndogo inayopepea ndani kwa ndani ili kukoleza moto huo wa mawe pindi unapowaka.

Dickson anasema, licha ya awali, kubezwa na familia yake na wanakijiji kwa kumuona anafanya vitu vya kitoto pindi alipoanza ubunifu wake, hakukata tamaa na hatimaye alifanikiwa kutengeneza jiko moja ambalo alilitumia kama mfano na kuanza kuzunguka nalo mitaani.