Myanmar:‘Mimi ni polisi lakini kamwe siwezi kuwafyatulia raia risasi’

Maelezo ya video, Baadhi ya maafisa wanasema sasa wako tayari kutumia silaha zao dhidi ya wenzao wa zamani.

Huku Myanmar ikielekea kwenye vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe, polisi wanakabiliwa na shinikizo kubwa kuamua ni upande gani wa kuutetea.

John ni mmoja wa maafisa 70 wa polisi ambao sasa wamejificha msituni baada ya kukataa kuwafyatulia risasi watu wanaopinga mapinduzi ya jeshi.

Baadhi ya maafisa wanasema sasa wako tayari kutumia silaha zao dhidi ya wenzao wa zamani. Kundi hilo limeipa BBC fursa ya nadra kwa mahojiano katika maficho yao