Virusi vya corona: Zanzibar yapinga kuwapa watu chanjo kisiri

Maelezo ya sauti, Virusi vya corona: Zanzibar yapinga kuwapa watu chanjo kisiri

Serikali Visiwani Zanzibar imekanusha taarifa kwamba wameanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona kimya kimya, Pamoja na kukanusha huko Waziri wa afya wa Zanzibar Nasor Ahmed Mazurui ameiambia BBC Mipango ya chanjo iliyopo mbali na uvumi huo.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amezungumza naye na kwanza alimtaka azungumzie kuhusiana na taarifa zinazozagaa kwamba wameanza kutoa chanjo kimya kimya.