Tundu Lissu amtaka Rais Samia kuanzisha mchakato wa katiba mpya Tanzania
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Tundu Lissu anayeishi ughaibuni amepongeza marekebisho kadhaa yaliyofanywa chini ya Rais wa awamu ya sita nchini Tanzania, Samia Suluhu Hassan japo angetamani kuona zaidi hasa katika kukutana na viongozi wa upinzani na kusukuma mbele mchakato wa Katiba Mpya.
Lissu ameiambia BBC wakati wa mahojiano mahususi na mwandishi Caro Robi kuwa masuala yaliyorekebishwa yako dhahiri.