Magari ya zamani yampa kijana fursa ya kuishi ndoto yake
Kijana wa Ktanzania Hussein Ngozi mwenye umri miaka 28 aliamua kuupiga teke ualimu aliosomea kwa takribani miaka mitatu na kuamua kujikita kwenye kufufua na kuyatengeneza magari ya zamani
Kwa kutumia pesa zake za mwisho za masomo ya elimu ya chuo kikuu Hussein alinunua gari aina ya Volkswageni beetle akinuia kuliweka kama kumbukumbu, lakini akiwa na gari hilo kwenye heka heka za kusaka ajira jijini Dar es salaam ndipo alipoiona fursa
Akiwa mkoani Iringa Mwandishi wa BBC Eagan Salla alizungumza naye na kuandaa taarifa ifuatayo