Picha za droni zafichua maisha kama ya binadamu ya nyangumi hatari zaidi

Maelezo ya video, Picha za droni zafichua maisha kama ya binadamu ya nyangumi hatari zaidi

Utafiti mpya ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Exeter na Kituo cha Utafiti wa Nyangumi unaonyesha nyangumi wauaji wanaweza kushirikiana kati yao kulingana na umri na jinsia, na nyangumi wadogo na wanawake wanapendana zaidi kuliko vikundi vingine.

Utafiti huo ulitumia kamera za ndege zisizo na rubani kusoma kundi moja la nyangumi wanaopishi kusini mwa pwani ya Marekani katika Jimbo la Washington, katika Bahari la Pasifiki. Karibu masaa 10 ya picha zilinaswa kwa siku 10.