Superdollar: Jinsi wahalifu wa genge lililosambaza dola bandia duniani walivyokamatwa
Dola bandia zenye ‘’thamani ya mamilioni’’ –lakini zinazoonekana kuwa halali- za noti za $100 zinaaminiwa kuwa zilikuwa katika mzunguko wa matumizi katika miaka ya 1990 na 2000. Maafisa wa Marekani wanasema zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara miongoni mwa wanadiplomasia wa Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini imekuwa ikikana shutuma kwamba imekuwa ikichapisha fedha bandia. Baada ya miaka minane ya upelelezi wa siri,FBI ilianzisha operesheni mbili katika wikendi mpoja- sherehe za harusi na talaka kwenye jumba la kifahari na safari ya boti zote zilipangwa ili kuwashawishi wahalifu kujitokeza kwa Marekani.
Operesheni hiyo ilifanikiwa- na watu themanini na saba wakakamatwa kwa ujumla. Noti mpya ya dola 100 ilitengenezwa upya mwaka 2013 katika jaribio la kuizuia kunakiliwa. Hatahivyo inaaminiwa kuwa idadi ndogo ya superdollar gushi bado zinaendelea kuzunguka hata leo.