Eid al-Fitr:Fahamu kwanini kuna Waislamu walioswali Eid jana na wengine wanafanya hivyo leo

Maelezo ya sauti, Mbona kuna mgongano kuhusu sikukuu ya Eid?

Kufuatia hali ya sintofahamu ya kutofautiana kuanza na kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani tulitaka kufahamu kutoka kwa Mussa Yusuph Kundecha ambaye ni mwenyekiti wa baraza kuu la Jumuiya na taaasisi za Kiislamu kujua mbona kuna mgongano wa siku ya Eid ambapo ni vigumu kwa Waislamu kusali Eid siku moja.

Kunao waislamu waliosherehekea Eid siku ya alhamisi na wengine wanaoswali leo Ijumaa