'Tutazingatia kuwa na sheria isiyokwaza ya upatikanaji na usambazaji habari'

Maelezo ya sauti, 'Tutazingatia kuwa na sheria isiyokwaza ya upatikanaji na usambazaji habari'

Wizara ya habari nchini Tanzania imesema kuwa iko tayari kupokea mapendekezo ya marekebisho ya sera na sheria ya habari kwa lengo la kutimiza azma ya uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, katibu wa mkuu wa wizara hiyo, Dk Hassan Abbas amesema ya kwamba serikali haitasita kufanya mabadiliko katika sheria au sera.

Kuhusiana na suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya habari, Abbas amesema ya kwamba wizara ya habari ipo tayari kuyasikiliza mapendekezo yaliyowasilishwa na chama cha wanahabari wanawake nchini humo TAMWA ili kuyashughulikia.

Regina Mziwanda amezungumza na Kajubi Mukajanga , Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania MCT , na kwanza anaanza kwa kuelezea walivyolipokea suala hilo.