Alichosema Mwinyi alipokutana na Rais Samia

Maelezo ya video, Alichosema Mwinyi alipokutana na Rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Sulu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi ambaye amempongeza akisema ameanza vizuri majukumu yake ya kuliongoza taifa hilo.

Mwinyi alisema lengo lake kufanya ziara hiyo lilikuwa kumjulia hali rais Samia na kumhakikishia msaada wowote atakaohitaji katika majukumu yake kama kingozi wa Tanzania.

Mwinyi aliwarai Watanzania kumuunga mkono rais Samia na kupeuka tofauti ambazo zitalirudisha nyuma taifa.