Virusi vya corona: Jinsi udhibiti wa vyombo vya habari ulivyotumiwa kukabiliana na janga hilo

Chanzo cha picha, CHINA NEWS SERVICE
Mwanzo wa mwaka 2020, serikali ya China ilikabiliwa na changamoto mbili kuu; ugonjwa usiojulikana ambao unatishia kuangamiza watu wake na wimbi la sauti mitandaoni ambalo lilielezea ulimwengu ni nini kinachofanyika.
Kufikia mwisho wa mwaka 2020, mtazamo katika vyombo vya habari vya China vinavyodhibitiwa na serikali unaonyesha kuwa changamoto zote mbili zinaonekana kuwa chini ya udhibiti.
Waandishi wa BBC Kerry Allen na Zhaoyin Feng wanaangazia jinsi wadhibiti wa maudhui mitandaoni walivyojitahidi kukabiliana na taarifa za ukosoaji, raia waliyojaribu kufikia maelezo yaliyofichwa na jinsi waendesha propaganda walivyobadilisha mtazamo wa umma kuhusu suala hilo.
Jaribio la awali la kuzima lawama na ghadhabu mitandaoni
Mwanzoni mwa mwaka, ilikuwa wazi kwamba kitu ambacho sio cha kawaida kilikuwa kinafanyika.
Maelfu ya jumbe zilisambazwa katika mitandao ya kijamii ya China, kuuliza serikali za mitaa ikiwa zinaficha virusi kama vya Sars.
Japo serikali inajulikana kuficha maudhui yanayosadikiwa kupinga serikali mitandaoni, katika mtandao kama wa Sina Weibo, maudhui kama hayo yalikuwa yakionekana.
Hii ni kwa sababu, wakati inapokabiliwa na janga kubwa, serikali ya China hukimbilia kuchukua hatua za moja kwa moja na wadhibiti wakati mwingine huchukua muda kufanya maamuzi.
Miezi ya Januari na Februari, vyombo kadhaa vya habari vilitumia fursa hiyo kuandaa taarifa za uchunguzi wa kina, ambazo zilisambazwa katika mitandao ya kijamii.
Baadaye, Beijing ilipopata mpango wa kuendesha propaganda, ripoti hizo zilipotezwa.
Lawama zilikuwa zikielekezwa kila upande. Katikati ya mwezi -Januari, Rais wa China Xi Jinping ghafla aliacha kuangaziwa katika vyombo vya habari vya China.
Hakuonekana hadharani, na picha zake zikatoweka katika ukurasa wa kwanza wa magazeti kama People's Daily. Kulikuwa na uvumi kuhusu kimya chake na kutoonekana kwake kulikuwa ishara ya wazi kwamba anajiepusha na lawama.
Ndani ya wiki moja hata hivyo, mambo yalibadilika.
Maafisa wa ngazi ya juu serikalini walianza kuonya mamlaka za mitaa kwamba ''zitasulubiwa kutokana na fedheha ya kihistoria'' ikiwa zitaficha maelezo kuhusu visa vya maambukizi katika maeneo yao.
Lawama zilianza kuelekezwa kwa uongozi wa Wuhan, huku magazeti kama Beijing News yakiandika uhariri na kuuliza, ''Kwa nini Wuhan haikujulisha umma mapema''.
Bw. Xi baadae akajitokeza hadharani mwezi Februari kama nguzo ya matumaini kuelekea uponyaji wa China.

Chanzo cha picha, SINA WEIBO
Udhibiti uliongezeka karibu na daktari
Katikati ya juhudi zote, ikawa wazi kuwa sauti ya mtu mmoja ilikuwa imenyamazishwa hali ambayo haikustahili kuwa.
Li Wenliang alijulikana kimataifa kama ''mfichua siri''- Daktari huyo aliyejaribu kuwaonya wenzake kuhusu virusi vinavyofanana na virus vya Sars. Dk. Li alifariki February 7 baada ya kubainika kwamba "alisumbua mpangilio wa kijamii" kwa "kutoa maoni ya uwongo".
Zaidi ya watumiaji million moja wa mtandao wa kijamii wa Sina Weibo waliandika ujumbe wa kumuunga mkono ulioambatanishwa na picha baada ya kifo chake, ambacho wengi walikitaja kuwa ''ukuta wa kilio'' cha China.
Hata hivyo jumbe hizo zimefutwa mitandaoni katika mazingira ya kutatanisha licha ya lalama za baadhi ya watu.
Watumiaji wa mtandao hata hivyo wamebuni njia za kumkumbuka daktari huyo kwa kutumia emojis, Morse code, and ancient Chinese script.

Chanzo cha picha, FACEBOOK
Wengine Pia wameandika ujumbe ambao hawawezi kuandika mtandaoni katika barakoa zao. Mwelekeo ulionekana kwenye Facebook na mtumaji maarufu wa WeChat wa watumiaji wakiandika maneno "siwezi kuelewa hii" kwenye barakoa zao kulalamikia kifo cha Dkt. Li.
Wanahabari 'kutoweka', na kupatikana tena nje ya China
Licha ya mamlaka kumtambua rasmi Dkt Li Wenliang kama "shahidi", wanaharakati kadhaa mashuhuri huenda wakafutwa katika historia ya Covid-19 ya nchi hiyo.

Chanzo cha picha, YOUTUBE/SCREENSHOT
Wakati wa mlipuko wa virusi Wuhan, wanahabari kadhaa raia wa China walichangia katika kupaza sauti kuhusiana na hali ilivyo kimataifa kufuatia jaribio la serikali la kutaka "kuficha" ulimwengu kilichokuwa kinafanyika katika mji huo.
Wanahabari hao ni pamoja na Chen Qiushi, Fang Bin na Zhang Zhan. Video zao zilitazamwa mara elfu kadhaa katika mtandao wa YouTube walipoamua kufahamisha ulimwengu yaliyokuwa yanajiri Wuhan.
Hata hivyo hatua hiyo ilikumbwa na changamoto zake. Kamati inayowalinda wanahabari ilisema kuwa mamlaka za Wuhan, '' ziliwakamata waandishi kadhaa wa habari kwa kuangazia masuala ambayo yalipinga msimamo rasmi wa jinsi Beijing ilivyokuwa inashughulikia janga hilo la kiafya''.
CPJ inasema watu kati yao na vituo vyao vya YouTube vilifungwa China, ni watu kidogo nchini wanajua athari za hatua hiyo.
Maswali pia yameibuliwa ikiwa mwanahabari mmoja ambaye alipatikana nje ya nchi baada ya kutoweka, ni sehemu ya kampeni za propaganda zinazoendelezwa ughaibuni.

Chanzo cha picha, Li Zehua/Youtube
Li Zehua alitoweka mwezi Februari baada ya kuweka video katika mtando wa YouTube akisema gari la polisi linamfuata.
Hakuna taarifa kumhusu ziliwahi kuangaziwa kwa miezi miwili, lakini baadae aliweka video nyingine mtandaoni akisema kuwa anashirikiana na mamlaka na kwamba yuko karantini.
Hajawahi kuweka ujumbe mwingine mtandaoni tangu wakati huo, baadhi ya watu wanahisi huenda alilazimishwa kuweka video hiyo.
Vijana wameteseka lakini wamepata njia mpya kuhakikisha sauti zao zinasikika

Chanzo cha picha, SINA WEIBO
Tangu mwezi Machi, China imekuwa ikitaka kujinadi kwa kuangazia ufanisi wake katika kukabiliana na virusi vya corona, lakini wadhibiti wa maudhui mtandaoni wamekuwa wakifuta mitandaoni ujumbe ambao unapinga ajenda hiyo, hususan miongoni mwa vijana.
China imesisitiza kuwa inataka kujiepusha na hatua ya kutotoka nje kama iliyochukuliwa Wuhan.
Lakini gazette la South China Morning Post linasema kuwa, vyuo vikuu vingi vimeendelea kuwekewa vikwazo vya kutotoka nje.
Mwezi Agosti, wanafunzi Wengi walirudi darasani kwa mara ya kwanza. Lakini maandamano yalitibuka katika vyuo vikuu tofauti nchini humo, wanafunzi wakilalamikia kupimiwa muda wa kutumia huduma za intaneti na kwa madai kwamba idadi ya wanaotumia huduma hiyo imeongezeka.
Hasira na kutoridhika miongoni mwa vijana wa China mwaka huu kumewafanya baadhi yao kuachana na majukwaa ya kawaida ya mitandao ya kijamii na kutumia njia zingine zisizokuwa za kawaida kuwasilisha video zao.












