Uteuzi wa Seif Sharif Hamad Zanzibar umepokewa vipi?
Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi amemteua Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Seif Sharif Hamad kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Katika gumzo tunajadili suala hili na mapokeo yake visiwani Zanzibar.
Awali Scolar Kisanga alizungumza na Said Msonga ambaye ni mchambuzi wa masuala ya siasa, Dkt Mzuri Issa Mkurugenzi wa chama cha waandishiwa habari wanawake Zanzibar ambaye pia ni mchambuzi wa siasa.
Anaanza kwa kuelezea hatua hii imepokelewaje visiwani humo.