Uchaguzi wa Tanzania una umuhimu gani kwa nchi jirani?

Maelezo ya video, Uchaguzi wa Tanzania una umuhimu gani kwa nchi jirani?

Tarehe 28 mwezi Oktoba, wananchi wa Tanzania (kote bara na visiwani Zanzibar) watachagua viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano ijayo.Uchaguzi wa mwaka huu unaonekana kuangazia masuala ya usalama wa kiuchumi na haki za binadamu. Rais John Pombe Magufuli wa CCM anawania urais kwa muhula wa pili ambapo anapingana na wawaniaji wengine 15 akiwemo mpinzani wake mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu.Kando na maendeleo, utawala wa rais Magufuli umekosolewa ndani na nje ya nchi kwa kuminya uhuru wa kujieleza, kukandamiza upinzani na kutoimarisha diplomasia ya kikanda na kimataifa. Lakini je, uchaguzi huu una umuhimu gani kwa mataifa jirani na ulimwengu kwa ujumla?Video ya George Wafula na Anthony Irungu.