Mke wa mwanaharakati wa Hong Kong aomba msaada mumewe aachiwe huru
Mwezi Agosti, wanaharakati 12 kutoka Hong Kong , walikamatwa na mamlaka za China baharini walipokuwa wakijaribu kutorokea Taiwan.
Ni jambo ambalo si la kawaida kutoroka mji ambao umekuwa na mzozo wa kisiasa. Sasa wanashikiliwa bila kushtakiwa nchini China.
Mke wa mwanaharakati mmoja amezungumza na BBC akitaka asitambulike akiogopa madhara yanayoweza kutokea.