Mdahalo wa Urais: Ukweli wa madai ya Trump na Biden

US President Donald Trump and Democratic presidential nominee Joe Biden participate in their first 2020 presidential campaign debate

Chanzo cha picha, Reuters

Rais Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden wamekabiliana kwa mara ya kwanza katika mdahalo wa kwanza kati ya mitatu itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni kabla ya uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba.

Wakati wa mdahalo huo uliochukua dakika 90, wagombea hao walikabiliana kwa kila jambo walilokuwa wanazungumzia kuanzia uchumi hadi namna ya kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Kitengo cha Reality Check BBC kimechambua baadhi ya madai hayo.

Section divider

Trump: "Tumeimarisha uchumi kwa kiasi kikubwa katika historia"

Uamuzi: Huo sio ukweli - kumekuwa na wakati katika historia ya Marekani ambapo uchumi umeimarika zaidi.

Kabla ya mlipuko wa virusi vya corona, rais Trump alidai kwamba uchumi umeimarika kuliko kipindi kingine chochote kile.

Ni kweli uchumi ulikuwa unafanya vizuri kabla ya janga la corona - ikiwa ni kile kilichokuwa kinaendelea wakati wa utawala wa Obama - lakini kuna wakati ambapo uchumi uliimarika zaidi.

Debate

Chanzo cha picha, Reuters

Section divider

Biden: "Tuna asilimia 4 ya idadi ya watu duniani, [lakini] asilimia 20 wamekufa"

Uamuzi: Hili huenda lina ukweli kwa kiasi fulani. Lakini ukiangalia idadi ya vifo ikilinganishwa kwa mtu mmoja mmoja, kuna idadi ya nchi ambazo ziko vibaya zaidi kuliko Marekani.

Bwana Biden amekosoa utawala wa Bwana Trump jinsi ulivyoshughulikia ugonjwa wa Covid- 19.

Kulingana na idadi hiyo, ni kweli. Marekani ina idadi ya watu milioni 328 ambayo ni asilimia 4 tu kati ya watu bilioni 7.7 duniani.

Joe Biden

Chanzo cha picha, Reuters

Kumekuwa na vifo 205,942 vilivyorekodiwa Marekani kutokana na virusi vya corona, kulingana na Chuo Kikuu cha John Hopkins. Idadi ya vifo vilivyorekodiwa duniani ni 1,004,808.

Katika hili, Marekani inahesabu asilimia 20 ya vifo kutokana na Covid-19 duniani, ingawa kuna tofauti kuhusu namna nchi zinavyoredi idadi idadi hiyo.

Section divider

Trump: ongezeko la upigaji kura kwa njia ya posta utasababisha "ulaghai ambao haujawahi kushuhudiwa"

Ukweli: utafiti haujabaini ushahidi wa kutokea kwa ulaghai ingawa kumekuwa na visa kidogo.

Kutokana na janga la virusi vya corona, idadi kubwa ya wapiga kura inatarajiwa kupiga kura kwa njia ya posta katika uchaguzi wa mwaka huu.

Rais ameonya mara kadhaa hili litasababisha kutokea kwa kiwango kikubwa cha udanganyifu.

Kumekuwa na visa kidogo vya udanganyifu ikiwemo mifano ya hivi karibuni huko North Caroline na New Jersey.

Donald Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Septemba, Idara ya sheria Marekani ilitoa taarifa kuhusu tukio la Pennsylvania ambapo "kura 9 za wanajeshi zilipatikana na kuharibiwa na kusema saba kati ya kura hizo zilikuwa zimepigwa kumuunga mkono Rais Donald Trump".

Lakini licha ya matukio hayo, utafiti uliofanywa mara kadhaa haujaonesha mapungufu makubwa ya kukithiri kwa udanyanyifu.

Kiwango cha ulaghai kwenye upigaji kura kwa jumla nchini Marekani ni kati ya asilimia 0.00004% na asilimia 0.0009, kulingana na utafiti wa mwaka 2017 wa kituo cha Sheria cha Brennan.

Section divider

Biden: "watu milioni 100 [Marekani] wanaugua magonjwa yanayowaweka katika hatari"

Uamuzi: hakuna jibu la moja kwa moja.

Wagombea hao walikabiliana kuhusu watu wangapi Marekani wenye magonjwa yanayowaweka katika hatari ambako kunaweza kusababisha baadhi yao wasiweze kupata huduma ya bima ya matibabu.

Bwana Biden alisema kulikuwa na watu milioni 100 ambao tayari wana maradhi mengine lakini rais Trump alisema kuwa idadi hiyo ni uongo mtupu.

Ni wangapi waliopo? Hakuna jibu sahihi.

Kulingana na Idara ya Afya na Huduma Marekani, kati ya watu milioni 50 na 129 ambao sio wazee tayari wana matatizo ya afya.

Mashirika mengine yana idadi tofauti. Kituo cha Maendeleo Marekani kinaamini idadi hiyo ni ya juu, watu milioni 135 wakiwa chini ya umri wa miaka 65.

Section divider

Trump: "Zimesalia wiki kadhaa kabla ya kupatikana kwa chanjo"

Ukweli: kuna uwezekano mdogo sana" wa kupatikana kwa chanjo kabla ya mwisho wa Oktoba, mshauri mkuu wa kisayansi kwa mpango wa chanjo wa Marekani amesema.

Moncef Slaoui alisema maneno hayo kwenye taarifa aliyoitoa mapema Septemba.

Wakati huohuo, Daktari Anthony Fauci, mtaalamu mkuu nchini humo wa magonjwa ya kuambukiza alitabiri kwamba Marekani itajua ikiwa imefanikiwa kupata chanjo salama kufikia Novemba au Desemba mwaka huu.

Akiwa kwenye kikao cha seneti mwaka huu alisema kuna uwezekano kuwa na chanjo ya kutosha kwa kila raia wa Marekani kufikia Aprili.

Section divider

Biden: "Sekta ya viwanda ilikuwa imekumbwa na uhaba wa fedha kabla ya virusi vya corona

Uamuzi: huo sio ukweli, kulingana na idadi.

Mgombea wa Democratic Joe Biden alipendekeza kwamba hata kabla ya Covid-19 "sekta ya uzalishaji ilikuwa imekumbwa na uhaba wa fedha".

Janga la virusi va corona liliathiri sekta hii. Kufikia Agosti, ajira katika sekta ya uzalishaji ilikuwa 237,000 nchini Marekani ikilinganishwa na kipindi Trump anaingia madarakani 2017.

Lakini kabla ya mlipuko wa virusi vya corona, Rais Trump alikuwa ameongeza ajira karibu nusu milioni katika sekta ya uzalishaji katika kipindi cha miaka mitatu ya kwanza akiwa madarakani.

Section divider

Biden: "Trump hajashusha bei ya dawa kwa yeyote yule "

Verdict: Gharama ya wastani kwa dawa ilishuka kidogo hadi Agosti 2019, ingawa ilianza tena kupanda.

Kwa mujibu wa ofisi ya takwimu za kiwango cha bei kwa watumiaji (CPI)- ambayo hutathmini kiwango cha gharama za bidhaa kwa kila nyumba Marekani - kiwango cha bei za dawa kilishuka Agosti 2019 kwa asilimi 0.3.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza gharama ya dawa kushuka kwa zaidi ya miezi 12 tangu mwaka 1973. Huku wastani wa bei ya dawa ukipanda kwa zaidi ya asilimia 1.5 mwaka uliofuata, chini ya Rais Trump wastani wa bei ukupanda umekuwa wa chini ukilinganishwa na enzi ya Obama.

Njia ya CPI si kwamba ndio njia sahihi ya kutathmini kiwango cha bei ya dawa kwasababu kinajumuisha tu dawa zinazotumika kwa wingi ambazo kawaida huwa ni za bei ya chini.