Virusi vya corona: Mbwa wa kunusa corona wapelekwa uwanja wa ndege wa Finland Helsinki-Vantaa

Maelezo ya video, Mbwa wa kunusa wanaobaini corona

Mbwa wa kunusa waliopewa mafunzo ya kubaini Covid-19 wamepelekwa uwanja wa ndege wa Finland Helsinki-Vantaa kusaidia kukabiliana na janga la corona. Majaribio yanafanyiwa abiria waliojitolea. Mtafiti anayeongoza utafiti huo anasema majaribio hayo yameonesha matokeo ya kufana lakini usahihi wa mbwa hao bado haujathibitishwa.