Moto wateketeza kambi kubwa ya wahamiaji Ugiriki

Maelezo ya video, Moto wateketeza kambi kubwa ya wakimbizi Ugiriki

Moto wateketeza kambi kubwa ya wahamiaji nchini Ugiriki, na maelfu wakusanyika katika kisiwa cha Lesbos.

Kambi hiyo ambayo ilikuwa karantini baada ya wahamiaji kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Vikosi vya zima moto vilipambana kuokoa maelfu ya wahamiaji.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.