Warohingya wengi wamekuwa wakimbizi baada ya kutimuliwa makwao

Maelezo ya video, Jinsi watoto wanaoishi kwenye kambi wanavyotamani hata kwenda nje tu

Miaka mitatu tangu walipokuwa wakimbizi, watoto Warohingya wanatamani hata kwenda mjini tu

Miaka mitatu iliyopita, kamata kamata iliyotekelezwa na jeshi la Myanmar kulisababisha maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kufariki dunia huku wengine wengi wakitoroka na kuingia Bangladesh.

Zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya sasa hivi wanaishi katika kambi kubwa ya wakimbizi ya Bazar, Bangladesh. Watoto wanaishi kwenye kambini wanatamani hata kutoka kwenda mjini tu.