BBC yagundua maasi ya Muungano wa nchi za kiarabu ndani ya Libya

Maelezo ya video, Droni za sumu za Libya

BBC imegundua ushahidi mpya kwamba kombora linaloongozwa, lilifyatuliwa kutoka ndege isiyo na rubani (Droni) ya UAE, na kuwauwa wanajeshi wakufunzi 26.

Muungano wa nchi za kiarabu UAE umekana kuingilia kati katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya. Lakini BBC imegundua ushahidi mpya kwamba kombora linaloongozwa, lilifyatuliwa kutoka ndege isiyo na rubani (Droni) ya UAE, na kuwauwa wanajeshi wanafunzi 26 ambao hawakuwa na silaha Januari 2020 .

BBC pia iligundua kuwa UAE ilipeleka droni zake na ndege nyingine za kijeshi ili kuunga mkono washirika wa Libya, na Msri kufuatia hatua ya UAE kutumia ngome zake za anga karibu la mpaka wa Libya.

Uchunguzi wa BBC Africa Eye na Idhaa ya BBC ya kiarabu ulibaini ushahidi mpya unaohusisha serikali ya Emirate katika mashambulio ya ndege zisizo na rubani dhidi ya shule ya mafunzo ya kijeshi ya Libya ambapo wanafunzi 26 waliuawa.