Watu 8 wameteuliwa kuwania wadhfa wa mkurugenzi mpya wa Shirika la biashara Duniani WTO
Watu nane wameteuliwa na nchi zao kuwania wadhifa huo, kupitia mfumo wa mahojiano na uteuzi.
Watatu kati yao wanatoka barani Afrika. Unaweza kujiuliza kwanini wadhifa wa mkuu wa shirika la biashara la kimataifa, WTO ni muhimu? Mhariri wa kitengo cha Biashara cha BBC Afrika, Zawadi Mudibo alizungumza na Waafrika wanaowania nafasi hiyo.