Rapa awa sauti ya wafanyikazi wahamiaji India

Maelezo ya video, Rapa awa sauti ya wafanyikazi wahamiaji

Rapper Dule Rocker amevuma mitandaoni nchini India kutokana na muziki wake unaoangazia hali ya wahamiaji wakati wa amri ya kutotoka nje kukabiliana na Covid-19. Umasikini umewalazimisha wasomi kutoka watu wa tabaka la chini kufanya kazi ya kupanguza meza. Kijana huyo kutoka tabaka la jamii ya Dalit sasa amerudi kijijini kwao katika jimbo la mashariki la Orissa (Odisha) ana imani kwamba ataendelea kutunga nyimbo za kuangazia watu wa kawaida katika jamii na changamoto wanazopiti.