Atamba kwa mtindo wake wa kipekee wa maonyesho ya fasheni za mavazi

Maelezo ya video, ‘Nilitamba mtandaoni na mitindo yangu ya fasheni’

Fashion Week au Wiki ya Fasheni ni sehemu muhimu ya sekta ya mitindo ya mavazi, lakini kutokana na Covid- 19, nembo mbalimbali za fasheni zilisitisha maonyesho yao. Lakini si mbunifu huyu wa mitindo. Anifa Mvuemba alijifunza binafsi fasheni ya 3D kwa kutumia Google, matokeo yake yalikua ni maonyesho yajayo ya maonyesho ya fasheni na yalisambaa sana mtandaoni.