Tanzania yafafanua agizo la TCRA kuhusu sheria mpya ya mawasiliano
Taarifa iliyotolewa na mamlaka ya mawasialiano nchini Tanzania TCRA, siku ya Jumatatu kuvitaka vyombo vya ndani kapata kibali cha kuwaruhusu kurusha matangazo kutoka vyombo vya habari vya kimataifa imeendelea kuzua mjadala ndani na nje ya nchi.
Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus amezungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Bw. Harison Mwakyembe na kwanza amemuuliza kama ni kweli vyombo vya utangazaji vinavyorusha matangazo kutoka nje ya nchini vitahitaji kibali kabla ya kurusha maudhui yake?