Uchaguzi Tanzania 2020: Tundu Lissu azungumzia kesi zinazomkabili
Suala hili limeibua hisia tofauti kuhusu hatima ya kiongozi huyo katika kinya'ng'anyiro cha urais ndani ya chama, muungano mwaka huu wa 2020 na siasa kwa ujumla.
Lissu amesema kuwa ana kesi za jinai sita katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kesi zote hizo Lissu amedai zinahusu ''maneno au kauli ambazo amezitoa ambazo zinakosoa au kuipinga au kutokukubaliana na sera, matendo au mipango ya serikali ya Tanzania''.